Nafasi Ya Matangazo

May 03, 2013

TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.

Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.

Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.

Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.

Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.

Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.

Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika. Timu nzima ya Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.
Posted by MROKI On Friday, May 03, 2013 3 comments

3 comments:

  1. AnonymousMay 04, 2013

    INASIKITISHA SANA, INAONEKANA ALIPOPANDA JUU KUPATA HEWA AKAPATWA NA KIZUNGUZUNGU NA PENGINE ALIKUWA KWENYE EDGE YA JENGO NDO AKADONDOKA, WHAT A SAD STORY. APUMZIKE KWA AMANI. AMINA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2014

    Jamani!! Poleni sana ndugu wa Shirima mliopatwa na Msiba huo. Siri yake anayeijua ni Mungu tu. Mungu amlaze mahali pema peponi Amen!!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo